Mfuko wa Shindano la Wajasiriamali Wachanga - KISWAHILI

Muhtasari

Wanawake na vijana ndio wanaoshikilia siku za baadaye na uti wa mgongo wa maendeleo ya kilimo. Kumekuwa na mwamko wa kufanya kilimo kama biashara katika siku za hivi karibuni ili kujenga thamani zaidi ya kiuchumi na kuwahamasisha vijana kujiunga na kilimo.

Kilimo kimepata msukumo kutokana na maendeleo ya haraka katika teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA). Katika nchi zinazoendelea, huduma za kifedha kwa njia ya simu zinaimarika. Vivyo hivyo, mitandao ya kijamii na programu huwasaidia wakulima kujua bei zilivyo sokoni au utabiri wa hali ya hewa. Katika nyakati hizi za COVID-19 wakulima hawa wanahitaji habari ambazo wanaweza kuziamini ili kuboresha maisha yao na kulinda familia zao.

Access Agriculture ni shirika lisilolenga faida ambalo linasaidia katika usambazaji wa video bora za mafunzo ili kushiriki maarifa ya kiutendaji kuhusu kilimo na usindikaji wa chakula katika maeneo ya Kusini mwa ulimwengu. Wakulima walio Amerika Kusini, Afrika na Asia wanaweza kujifunza kutoka kwa wenzao katika mabara mengine.  

Access Agriculture imebuni wazo la Entrepreneurs for Rural Access yaani Wajasiriamali kwa Ufikiaji wa Vijiji, ambao ni watu binafsi au kundi dogo la watu ambao hutumia ‘projecta janja’ kubuni au kukuza biashara zao. Kupitia mpango huu, Access Agriculture huwaomba vijana kupendekeza mawazo bunifu ya kuanzisha biashara, au kupanua huduma zao zilizopo, zinazohusiana na usambazaji wa video za kilimo.
Kupitia ruzuku inayotolewa kwa njia shindani, wajasiriamali wachanga wanaohamasisha na kuonesha tija watapokea projekta janja ya Digisoft (angalia picha hapa chini).

Kwa kutegemea ujuzi wa TEHAMA na mitandao ya vijana wa kiume na wa kike, tunaamini kwamba tunaweza kuwasaidia wakulima vizuri zaidi na kufanya kilimo hai kiwe cha kuvutia zaidi kwa vijana na kuwafikia wanawake wengi..


Project Janja za Digisoft

smart projector

Projekta janja ina video zote za Access Agriculture unazoweza kucheza bila muunganisho wa intaneti, bila umeme na bila mtandao wa simu. Inakuja ikiwa na kipokeaji cha umeme wa jua, betri na mfumo wa sauti unaofaa hadi watu 150 - vyote hivi katika mkoba mmoja au kasha thabiti.
Projekta hii hufanya kazi kama toleo la wavuti nje ya mtandao, huku video zikichaguliwa kulingana na vipengele au lugha. Maudhui haya husasishwa mara kwa mara.

Unaweza kuona video kuhusu projekta janja hapa:
Play smart… with the DCS smart projector
On the road with the smart projector - GADC Uganda
Farmers like videos from other countries
Entrepreneurs for Rural Access - India

Bofya hapa ili upate maelezo zaidi kuhusu projekta janja.


Maswali yanayoulizwa sana

Je, nitapata faida gani nikishinda?

Access Agriculture itakupa projekta janja kwa mkopo wa miezi 18, baada ya hapo projekta itakuwa yako ilimradi tu ujitolee kuwa kwenye mpango wa mafunzo na uwasilishe ripoti zinazohitajika. Access Agriculture itagharimia usafirishaji na ushuru wa forodha. Access Agriculture ina timu inayojituma itakayokufundisha, kukuelekeza na kukusaidia. Watakushauri jinsi ya kutumia projekta janja na wakusaidie kuandaa mipango yako. Pia utaunganishwa na wajasiriamali wengine wachanga ili kuwaruhusu kubadilishana uzoefu na kuimarisha au kutanua wigo wa shughuli zako.

Nitasubiri muda gani kabla ya kupokea projekta janja?

Ndani ya miezi 2-3 tangu unapopokea habari za kuwa mshindi, utahudhuria kikao cha mafunzo ambapo utapokea projekta janja.

Nisipotimiza vigezo vya kushiriki shindano, ninaweza kununua au kupangisha projekta janja?

Iwapo hutumizi vigezo, au usipochaguliwa kuwa mmoja wa washindi, unaweza kuwasiliana na Digisoft Education (info@digisoft-education.com) ili ununue projekta yako mwenyewe. Hamna chaguo la kupangisha.

Je, ninaweza kuwasilisha ombi ambalo tayari lilikuwa limetekelezwa na wengine?

Hapana. Tunatafuta mawazo asili kutoka kwa watu binafsi au vikundi, siyo yale yanayoiga kile ambacho wengine tayari wanakifanya.

Je, ninaweza kuwasilisha ombi lenye wazo ambalo tayari ninalitekeleza?

Ndiyo, tunakuhimiza upanue wigo wa shughuli au huduma zako za sasa.

Ninaweza kutuma maombi mangapi?

Unaweza tu kuwa sehemu ya ombi moja.

Ni kitu gani hakigharimiwi?

  • Tasnifu au utafiti wa kimasomo
  • Maombi ambayo yanahimiza utumiaji wa viuatilifu
  • Gharama za wafanyakazi au usafiri

Call for Proposals

South Africa

(Limpopo and Eastern Cape Provinces)

Can you come up with a business plan to provide agricultural video services to local farmers?

THIS CALL IS NOW CLOSED

Cameroon

Can you come up with a business plan to provide agricultural video services to local farmers?

THIS CALL IS NOW CLOSED

Uganda

(Karamoja region)

Can you come up with a business plan to provide agricultural video services to local farmers?

THIS CALL IS NOW CLOSED

India

Can you come up with a business plan to provide agricultural video services to local farmers?

Are you based in Andhra Pradesh or Telangana?

THIS CALL IS NOW CLOSED

Egypt

Can you come up with a business plan to provide agricultural video services to local farmers?

THIS CALL IS NOW CLOSED

Information about this call is only available in arabic.

Rwanda

Can you come up with a business plan to provide agricultural video services to local farmers?

THIS CALL IS NOW CLOSED

Zambia

Can you come up with a business plan to provide agricultural video services to local farmers?

THIS CALL IS STILL CLOSED

Tanzania

Can you come up with a business plan to provide agricultural video services to local farmers?

THIS CALL IS NOW CLOSED

Kenya

Can you come up with a business plan to provide agricultural video services to local farmers?

THIS CALL IS NOW CLOSED

To read more about Entrepreneurs for Rural Access, please click here