Kuhusu Mradi wa GIZ KCOA
Wito huu wa Entrepreneurs for Rural Access (Wajasiriamali kwa Ufikiaji wa Vijiji) ni sehemu ya mradi wa Vituo vya Maarifa ya Kilimo Hai (KCOA) Afrika unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani, GIZ. Ni sehemu ya mpango wa “Dunia Moja - Bila Njaa” wa Wizara ya Serikali ya Ujerumani ya Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo (BMZ). KCOA inatekelezwa katika maeneo yote ya Afrika kupitia vituo vya maarifa na washirika. Awamu ya kwanza ilianza mnamo 2019 na itaisha 2023. Lengo la jumla ni kuanzisha mkakati bunifu wa kukuza kilimo hai kote barani Afrika.
Sasa tunawomba vijana nchini Tanzania wapendekeze mawazo bunifu ya kuanzisha biashara, au kupanua huduma zao zilizopo, kuhusiana na usambazaji wa video za kilimo kwa kutumia Projekta Janja ya Digisoft.
Bonyeza hapa upate maelezo zaidi kuhusu projekta janja. |
|
Vigezo vya kushiriki
Waombaji: mtu mmoja au timu za hadi vijana 3 wanaweza kuwasilisha pendekezo
Umri: Miaka 18-30
Nchi: Wanaoishi Tanzania
Tarehe ya Uwasilishaji: Makataa ya kuwasilisha ni 10 Mei 2021
|
|
Miongozo na makataa kwa ajili ya pendekezo
- Watu binafsi au timu za hadi watu 3 wanaweza kuwasilisha pendekezo
- Mtu yeyote anaweza tu kuwa sehemu ya pendekezo moja
- Uwasilishaji wa mapendekezo ni kupitia mfumo wetu wa mtandaoni pekee
- Hamna barua pepe wala aina nyingine ya maombi yatakubaliwa
- Unatakiwa kuwasilisha hoja kuu za pendekezo lako la biashara jinsi ilivyobainishwa katika fomu ya uwasilishaji
- Mapendekezo yanatakiwa kuwasilishwa kufikia tarehe 10 Mei 2021
Kwa ufafanuzi zaidi, tafadhali angalia FAQs hapa kabla ya kuonana na Mratibu: jane@accessagriculture.org
Hatua za kufuata ili uwasilishe fomu ya ombi
- Soma mwongozo wa kutuma ombi: Usome kwa makini maagizo ya kutuma ombi pamoja na Maswali Yanayoulizwa Sana. Bonyeza hapa uone Maswali Yanayoulizwa Sana. Tafadhali angalia FAQs hapa.
- Jaza fomu ya maombi: Ili kufungua fomu ya maombi bonyeza “Tumia Ombi Mtandaoni”. Jaza taarifa zinazohitajika katika kila ukurasa. Unaweza “Kuhifadhi” fomu na kuihariri au kuikamilisha baadaye. Ni sharti ujibu maswali yote kabla ya kutuma ombi.
- Hakiki fomu: Nenda kwenye ukurasa wa mwisho kisha ubonyeza “hakiki”. Taarifa zote ulizojaza zitaonyeshwa na unaweza kuzisoma kabla ya kuwasilisha. Ikiwa unataka kubadilisha unaweza kubofya “ukurasa uliotangulia” ili urudi kwenye fomu.
- Tuma fomu: Ukishamaliza kujaza taarifa zinazohitajika, nenda kwenye ukurasa wa mwisho, bonyeza “hakiki” kisha bonyeza “wasilisha”. Fomu itawasilishwa na haiwezi kuhaririwa tena.
- Tafadhali kumbuka: Fomu ambazo hazijakamilika hazitazingatiwa - na kumbuka kuwasilisha ombi lako kabla ya tarehe ya mwisho.
- Uthibitisho wa barua pepe: Baada ya kuwasilisha fomu hiyo, angalia ujumbe wa kuthibitisha kupokelewa kwa ombi kwenye folda ya kikasha/taka/barua taka.
|
|
Maswali ya kujibiwa kwenye fomu ya maombi
Tunashauri utafakari kila swali lililo hapa chini na uandae majibu ya maswali.
- Ni kipi kimekuhamasisha kutuma ombi kwenye shindano hili? (Usizidi maneno 100)
- Je, unadhani ni tatizo au matatuzo gani katika jamii yako utayatatua kwa kutumia projekta janja na kuonyesha video? (Usizidi maneno 100)
- Una mpango gani wa kupata hela katika maeneo ya mikoani ukitumia projekta janja? (kwa maneno mengine, unapanga kupata hela vipi kutokana na projekta mahiri) (usizidi maneno 250)
- Je, hadhira unayolenga/wateja wako watarajiwa ni kina nani (miradi, vikundi vya wakulima, mashirika, watu binafsi)? (Usizidi maneno 100)
- Je, unatarajia kuwafikia wakulima wangapi katika vijiji vya jirani kila mwezi kwa ajili ya kuwaonyesha video? (Usizidi maneno 100)
- Utatumia mkakati gani kufikia idadi ya wakulima uliyotaja? Utawahamasishaje wakulima hawa kutazama video? (Usizidi maneno 250)
- Utawafikiaje vijana na wanawake katika jamii unazolenga? (Usizidi maneno 100)
- Ikiwa tayari una biashara, ni vipi projekta itaongeza thamani katika biashara yako ya sasa? Kama ni biashara mpya, ni huduma gani nyingine zinazohusiana unaweza kutoa kwa walengwa pamoja na kutazama video? (Usizidi maneno 250)
- Je, ni vipi utashiriki uzoefu wako wa kutumia projekta janja na Access Agriculture? (Usizidi maneno 100)
|
|
Mchakato wa uteuzi
- Kamati ya wafundishaji wa ERA, wataalamu wa mawasiliano na maendeleo watahakiki na kutathmini mapendekezo kulingana na upya na ubora wa pendekezo katika kukuza kilimo hai kwa kutumia video za Access Agriculture.
- Orodha fupi ya waombaji waliochaguliwa awali itaandaliwa na kamati hiyo.
- Waombaji waliochaguliwa awali watajulishwa kupitia barua pepe na/au simu.
- Kutakuwa na usaili mtandaoni kwa waombaji walioteuliwa.
- Waombaji waliochaguliwa watajulishwa kuhusu matokeo ya usaili ndani ya wiki moja baada ya usaili.
- Washindi wanne (4) watachaguliwa katika kila nchi.
- Washindi waliochaguliwa watakuwa na mkutano wa ana kwa ana na mfundishaji wa ERA ili kufafanuliwa majukumu na namna ya kuripoti lakini pia, kukabidhiwa projekta janja.
|
|
Matakwa ya utekelezaji kwa washindi
- kiwa wewe ni mshindi, utatarajiwa kusaini hati ya maadili ambayo inabainisha kwamba utaendelea kutumia projekta janja kuonyesha video za Access Agriculture kwa angalau miezi 18 ili kukuza biashara au huduma zako, kuhamasisha kuhusu kilimo hai na ikilojia ya kilimo na kutoa ripoti kwa Access Agriculture mara kwa mara. Baada ya miezi 18, projekta itakuwa mali yako.
- Washindi wote wanatakiwa kuanza shughuli ndani ya miezi 3 baada ya kupokea Projekta Janja. Access Agriculture ina haki ya kuchukua projekta janja ikiwa mhusika atashindwa kufanya shughuli.
|
|
Ikiwa ungependa ufafanuzi wowote, tafadhali kwanza angalia Maswali Yanayoulizwa Sana hapa (yatafunguliwa katika ukurasa mpya).
Iwapo bado una maswali, tafadhali wasiliana na Timu ya ERA katika eneo lako: jane@accessagriculture.org