Ufundishaji wa kilimo asilia shuleni

Ili kuthamini utamaduni wa wenyeji, na kuhimiza ukumbatiaji wa mtindo wa maisha wenye afya, ni muhimu shule zijumuishe mada kuhusu kilimo na chakula cha kiasili katika mtaala na shughuli zake zote. Kubuni vipengele vinavyohusiana na kilimo asilia katika mtaala wa shule kwa madarasa yote. Kwa kupanga ziara za shambani, watoto wanaweza kujifunza kutoka kwa wakulima kuhusu aina za kienyeji, shughuli za kiasilia za upanzi na vifaa vya kilimo. Unaweza kutenga chumba maalum kwa ajili ya utamaduni wa shambani wa wenyeji ambapo watoto wanaweza kusoma vitabu, kutazama video, kuonyesha kazi zao za sanaa na kucheza michezo.

Current language
Kiswahili
Need a language?
If you would like this video translated into other languages, please contact kevin@accessagriculture.org
Translated in
KENYA
Translation funded by
GIZ-KCOA
Uploaded
6 months ago
Duration
14:23
Produced by
Agro-Insight