Uvunaji na uhifadhi wa bamia

Vuna bamia laini kila baada ya siku mbili, ili zisiive. Lakini acha zile ndogo ili uzivune katika mkumbo unaofuata. Ikiwa utaacha maganda/matunda kwenye mbamia hadi yaive, matunda hayo yatatumia nguvu nyingi za mti huo na kupunguza kasi ya ukuaji. Mbamia ambao huvunwa kwa kisu hutoa maganda kwa hadi miezi 6 bila kukumbana na madhara. Bamia freshi zinaweza kuhifadhiwa kwa muda wa hadi wiki tatu kwenye friji ya jangwani bila kuharibika. Kwa kukata na kukausha bamia kwenye kivuli, zinaweza kuhifadhiwa kwa mwaka mmoja bila kupoteza virutubisho wala rangi yake halisi.

Current language
Kiswahili
Need a language?
If you would like this video translated into other languages, please contact kevin@accessagriculture.org
Translated in
KENYA
Translation funded by
GIZ-KCOA
Uploaded
10 months ago
Duration
11:51
Produced by
AMEDD