Kudhibiti sumu kuvu katika mahindi kabla na wakati wa kuvuna
Uploaded 5 years ago | Loading
14:00
Kwa kudumisha rutuba shambani mwako na kupanda mapema, mimea yako itakuwa na nguvu na haitaathiriwa sana na wadudu au kuvu. Mara baada ya mahindi yako kukauka na maganda yangali meupe, yavune ndani ya wiki moja au mbili. Kamwe usiweke mahindi unayovuna ardhini, la sivyo kuvu zitaingia kwenye mahindi yako na kuyaharibu unapoyahifadhi. Choma mahindi yote yaliyoharibika. Kamwe, usiyatumie kama chakula cha mifungo.
Current language
Kiswahili
Produced by
Agro-Insight