Dawa za miti shamba za kuwazuia wadudu
Uploaded 1 year ago | Loading
14:38
Baadhi ya mimea katika hali yake huwafukuza wadudu. Ikuze baina ya mimea yako kuzuia wadudu. Kwa kujua mimea mwitui inayokua eneo lako, unaweza kutengeneza dawa yako ya kuwazuia wadudu bila gharama. Ongeza mkojo wa ng’ombe kusaida kutoa maji ya maziwa kutoka kwenye matawi hayo ya mpira, matawi machungu na yenye harufu. Ni vizuri kubadilisha aina mbili ya dawa kienyeji ya kuzua wadudu. Andaa aina ya pili ya dawa ya kuwazuia wadudu na chepe ya tangawizi, kitunguu saumu na pilipili.
Current language
Kiswahili
Produced by
Green Adjuvants