Kubadilisha taka ya kuku kuwa mbolea
Uploaded 1 year ago | Loading
16:10
Uchafu wa kuku una nitrojeni na virutubishi vingine na ni nzuri kwa vijidudu vilivyopo mchangani. Ichanganye na samadi ya ng’ombe iliyooza na raslimali zenye viwango vya juu vya kaboni. Kuharakisha zoezi la kuoza, nyunyiza raslimali ya kuozesha asilia au Trichoderma kwa mchanganyiko huo. Kutokana na mayai yaliyooza, unaweza kutengeneza kichocheo cha ukuaji wa mimea kutokana na mayai yaliyoharibika, kwa kuiweka kwenye jagi na sukari nguru na maji ya limau / ndimu.
Current language
Kiswahili
Produced by
Green Adjuvants