Ugeuzaji wa mabaki ya samaki kuwa mbolea
Uploaded 1 year ago | Loading
15:20
Matumbo, vichwa, ngozi au sehemu nyingine yoyote ya samaki ambayo binadamu hali, inaweza kugeuzwa mbolea isiyo na kemikali kwa kuiacha ichache au kuvunda. Mabaki ya samaki yamesheheni naitrojeni, fosiforasi, kalsiamu na vitamini. Kwa kutumia mbolea ya samaki, tunaweza kuongeza vijidudu vyenye manufaa kwenye udongo, na hivyo basi kuufanya udongo huo kupata rotuba nayo mimea ipate virutubisho kwa urahisi. Hii inafanya mimea kukuza mizizi imara na majani kunawiri, ili kustahimili magonjwa na wadudu na kuzaa zaidi. Mbolea ya samaki inazidisha ubora wa mimea.
Current language
Kiswahili
Produced by
Green Adjuvants