Kuandaa kitalu cha miche ya pilipili
Uploaded 4 years ago | Loading
13:34
Chora mitaro isiyo na kina kirefu ukitumia kijiti. Mitari inafaa kuwa sambamba na upande mfupi wa kitalu na iachane kwa sentimita 15.Weka mbegu chache kwenye kila mtaro. Ukitumia mbegu nzuri, karibu kila mbegu itaota, kwa hivyo hakikisha unaacha nafasi ya kutosha kati ya kila mbegu.Usiweke mbegu nyingi mno kwa sababu utaishilia kuwa na miche mirefu, myembamba isiyothabiti.Mbogamboga nyingi huwa na mbegu ndogo zinazofaa kupandwa juujuu ya ardhi. Rashia udongo laini ili kufunika mbegu .
Current language
Kiswahili
Produced by
Agro-Insight