Jinsi ya kutengeneza chumba-baridi cha nyanya
Uploaded 2 years ago | Loading
5:44
Unapovuna nyanya zako, ikiwa unataka kuzihifadhi kwa muda mrefu, unafaa kutafuta njia ya kupunguza kiwango cha joto. Kwa kuwa kupata umeme vijijini kunaweza kuwa tatizo, ni lazima utafute njia za kupunguza kiwango cha joto la zao hili ambalo huharibika haraka. Baadhi ya wakulima kutoka Dambatta, Jimbo la Kano, nchini Nigeria wametumia matofali ya kawaida ya udongo kutengeneza chumba-baridi chenye ufanisi mkubwa.
Current language
Kiswahili
Produced by
Countrywise Communication