Kuikuza nafaka kwa ajili ya kuilisha mifugo
Uploaded 1 year ago | Loading
14:58
Reference book
Nafaka zikiwekwa kwenye maji kwa muda na kuachwa ziote, zitatoa mashina michipuko. Kwa kufyonza maji, mbegu zilizomea zinaongeza uzito wake maradufu. Michipuko ni rahisi kusagika/kumeng’enywa kuliko nafaka yenyewe, kwa sababu uchipukaji huo unabadilisha karibu kirutubisho kizima cha wanga kwenye nafaka kuwa sukari. Pia hufanya madini, vitamini, na protini nyingi kupatikana kwa wingi.
Current language
Kiswahili
Produced by
Atul Pagar, Govind Foundation