Kitalu cha vitunguu
Uploaded 4 years ago | Loading
12:37
Miche ya vitunguu inahitaji mchanga wenye afya ,na haujashikamana. Katika msimu wa mvua unahitaji kuinua kitalu ili mizizi ya vitunguu yasioze. Ongeza mbolea iliyokomaa au mboji. Ukitumia mbegu bora, mbegu nyingi zitakua na utahitaji kiwango kidogo. Mbegu za vitunguu zinahitaji nafasi kukua, kwa hivyo usizipande karibu sana. Weka mbegu katika mistari, sentimita 5 hadi 10 kando na sentimita 1 kwa kina. Funika mbegu polepole na mchanga mzuri.
Current language
Kiswahili
Produced by
Agro-Insight